
Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani nje
kidogo ya mji wa Zanzibar, Naibu Waziri wa habari ,Utaliii ,Utamaduni na
Michezo Chumu Kombo amesema Serikali kupitia mradi wa matokeo kwa
ustawi imekusudia kuvitumia visiwa hivyo katika kukuza sekta ya utalii.
Amesema miongoni mwa visiwa mbavyo vimo katika mradi huo ni pamoja na
kisiwa kilichopo Tindini, Unguja Ukuu, Kaepwani na Kikungwi.
Amesema wananchi watakapokuwa na muamko wa kutumia mradi huo kwa
kuanzisha shughuli na Bidhaa za kitalii kutokana na rasilimali zilizopo
Nchi itawasaidia kupunguza ugumu wa maisha pamoja na kupunguza tatizo la
ajira kwa vijana.
Amesema serikali kupitia mabaraza ya utalii imefanya tathmini kwa
visiwa hivyo juu ya matumizi sahihi yaliyokusudiwa ili kuendana na mila
na desturi ya Kizanzibari.
chanzo: Zanzibar24.
Comments