Vijana waendelea kusherehekea miaka 41 ya kuzaliwa chama cha CCM Unguja.

Related imageUmoja wa Vijana wa CCM Tawi la Nyerere “A” Jimbo la Magomeni wameendelea na sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa Chama chao kwa kufanya Bonanza la Michezo mbalimbali Jimboni humo.
Bonanza hilo lilifanyika kwa lengo la kuimarisha afya na mashirikiano miongoni mwa Wanachama wa CCM na jamii kwa ujumla.
Akizungumza katika Bonanza hilo Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi amesema ili kuweza kukienzi na kuendeleza matunda yaliyoachwa na waasisi wa chama hicho ni vyema Vijana wakaendeleza mabonanza hayo.
Amesema Vijana wa chama cha Mapinduzi wanapaswa kujifunza kutoka kwa vijana wengine wa chama hicho kwa kuandaa sherehe maalum ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi.
Amesema fursa hiyo itawafanya vijana hao kufuata nyayo za waasisi wa chama hicho kwani ulikuwa ni utaratibu wao kufurahia kila ifikapo siku ya kuzaliwa chama hicho.
Aidha aliwapongeza sana Vijana kwa kuandaa michezo mbali mbali kwa kutambuwa kwamba michezo ni njia moja wapo ya ajira yao hivyo, aliwaomba wazazi kuwaruhusu watoto kushiriki katika suala la michezo.
Katika risala ya Umoja wa vijana wa tawi la Nyerere “A” wamesema wameamuwa kusheherekea sherehe za kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ili kuweka mashirikiano na wenzao katika bonaza la michezo waliloliandaa.
Vijana hao pia waliomba kutengenezewa barabara za ndani za Jimbo hilo sambamba na kupatiwa usafiri wa utakaotumika kwa matumizi mbalimbali katika Jimbo napia kuboreshewa Afisi yao na kupatiwa vifaa vya kufanyia kazi ili kuweza kujiajiri wenyewe.
Sherehe hizo zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana wa tawi la Nyerere “A” Jimbo la magomeni na kuambatana na michezo mbalimbali kama Nage, uvutaji wa kamba,ukunaji wa nazi na mbio za miguu miwili.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar. 
chanzo:Zanzibar24.

Comments