
Akichangia hutuba ya uchumi,mpango wa Maendeleo na mwelekeo wa bajeti kwa mwaka 2018/19 mwakilishi huyo amesema sekta ya kilimo inahitaji mashirikiano makubwa kati ya wakulima ,Serikakli na watu binafsi ili kuwawezesha wakulima kufikia malengo waliyoyakusudia.
Amesema uhaba wa matrekta katika sekta ya kilimo bado ni tatizo kubwa jambo ambalo linawapa usumbufu mkubwa wakulima katika kufikia kilimo cha Chakula na biashara.
Amesema watu wenye uwezo wakiengeza bidiii katika kuwekeza kwenye sekta ya kilimo itawasadia kunufaika na kilimo cha ndani ya nchi pamoja na kuwezesha serikali kufikia Uchumi wa kati utakao punguza kasi ya umaskini nchini.
Aidha amewata wakulima kutokata tama katika kilimo badala yake waengeze bidiii ili kuepusha kuagizia vyakula kutoka Nnje ya nchi.
chanzo:Zanzibar24.
Comments