UAE kuwajengea nyumba waliopata maafa Zanzibar.

Serikaliya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini naSerikaliya Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), kuhusiana na ujenzi wa nyumba kwaajili ya wananchi ambao makaazi yao yaliharibika kutokana namvua zamasika.

Hafla sainihiyo imefanyika katika Ofisiya Makamu wa Pili kati ya Mamlaka ya Mwezi Mwekundu ya UAE itakayoshughulikia ujenzi huo na Kamisheni ya Maafa ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed, amesema msaada waujenzi hayo ni imatunda ya ziara iliyofanywa na RaisDk. Ali Mohamed Shein katika Falme za Kiarabu wiki kadhaa zilizopita.

Katikaziara hiyo, Mfalme wa UAE aliahidi kuisaidia Zanzibar katika sektambalimbali zamaendeleo nahuduma zakijamii.

“Tunaishukuru Serikaliya UAE kwa msaada huu mkubwa ambao utazidikuimarisha uhusiano naudugu uliopo baina yanchi zetu,”alisema Aboud.

Nae Mkurugunzi wa Kamisheni ya kukabiliana na Maafa Shaaban Seif Mohammed, amesema msaada huo utasaidia kuondoa usumbufu wanaopata wananchi katika kipindi cha mvua hasa yanapotokea mafuriko.

“Wananchi wanaoishi maeneo ya Ziwa Maboga, Mwanakwerekwe namengine yanayotuwama maji ndio watakao hamishiwa kwenye nyumba hizo ili wakae katika makaazi salama,” alisema.

“Aidha nyumbazilizojengwa katika maeneo yenyekupita au kukaa maji tutazivunja ili kukomesha maafa nausumbufu,”alielezaMkurugenzihuyo.

Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari zamapema kwakuondoka maeneo yanayokaa maji ilikuepukana na hasara namatatizo wakati wakipindi cha mvua.

Nae mwakilishi kutoka ubalozi wa UAE Mohammed Ibrahim Al-Bahr, amesema Serikali yanchi yake itaendelea kuisaidia Zanzibar kwakuimarisha huduma zakijamii ikiwemo hospitali nauchimbaji wa visima kwalengo la kuwasaidia wananchi wake pamoja na kuleta maendeleo.

Ameishukuru Serikali ya Zanzibar kwakuwapatia ardhi itakayotumika kujenga nyumba za makaazi ya kudumu kwaajili ya wananchi waliokumbwa namaafa ili waishi kwafuraha nautulivu.

Mradihuo utahusisha nyumba 55 ambapo 30 zitajengwa Fukuchani Mkoa waKaskazini Unguja, nanyengine 25 zitajengwaTumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba.
chanzo: Zanzibar24.

Comments