Thamani ya sarafu ya Afrika Kusini yaporomoka, ANC kumuondoa Zuma ofisini kwa nguvu.

Thamani ya sarafu ya Afrika Kusini yaporomoka, ANC kumuondoa Zuma ofisini kwa nguvuThamani ya sarafu ya Afrika Kusini (rand) imeporomoka baada ya chama tawala nchini humo ANC kutishia kuwa kitamuondoa ofisini kwa nguvu Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo.

Habari zinasema dola moja ya Marekani imeuzwa kwa kati ya rand 11.95 na 11.99 kutoka 11.8 jana Jumatatu. Wakuu wa ANC wanatazamiwa kufanya kikao na waandishi wa habari hii leo ili kuweka wazi maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho tawala.
Hata hivyo vyanzo vya habari vimearifu kuwa, Zuma amepewa masaa 48 awe ameachia ngazi, baada ya kufanyika mkutano wa dharura wa chama tawala ANC.
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa, Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa amemkabidhi Zuma ilani ya kujiuzulu baada ya kumalizika kikao cha jana cha Baraza Kuu la ANC.
Uamuzi wa jana umefikiwa baada ya Zuma na Ramaphosa kufanya mazungumzo ya siku tano kuhusu hatima ya Rais huyo wa Afrika Kusini anayeandamwa na kashfa za ufisadi, bila kufikia natija yoyote.
Iwapo Jacob Zuma atajiuzulu, Cyril Ramaphosa ambaye ni makamu wake atachukua uongozi wa Afrika Kusini hadi utakapoitishwa uchaguzi mwingine wa rais kati kati ya mwaka ujao 2019.
chanzo:parstoday.

Comments