
“Nilisikia mchezaji bora wa Afrika kutoka Tanzania Mbwana
Samatta anacheza Genk, hii ni nchi ya mpira licha ya changamoto za
shirikisho siku za nyuma lakini kwa sasa mpo kwenye mstari kutokana na
uongozi mpya kwa kushirikiana na CAF pamoja na FIFA” Gianni Infantino.
“Tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kuleta maendeleo ya
mpira, leo tumeileta dunia Dar es Salaam tuna wageni kutoka Asia,
America ya Kaskazini, Carebean, Afrika na Fifa tupo hapa kwa hiyo
ulimwengu upo hapa leo na nina furaha kwa hilo.”
Kama unakumbuka, Samatta alishinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Afrika) mwaka 2015 akiwa mchezaji wa
TP Mazembe kabla hajajiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji anayoitumikia
sasa.
chanzo: zanzibar24.
Comments