
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu wakaribu na eneo la tukio
ikithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hasina
Ramadhan Tawfik amemtaja marehemu huyo kuwa ni Tatu Makame Hajji ambapo
majira ya saa nne dakika thelathini asubuhi marehemu kabla hajapatwa na
ajali hiyo alikua akienda kazini ambapo alikuwa njiani kuelekea huko
ndipo aliponasa katika waya wa umeme ambayo nguzo yake imekatika.
Kufuatia kutokea kwa tukio hilo Kamanda Hasina Ametowa wito kwa jamii
kuwa makini wakati wanapokuwa katika shuhuli zao ili kujiepusha na
majanga kama hayo.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi Hospitali na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.
chanzo: zanzibar24.
Comments