Mwanamuziki maarufu ahukumiwa kwa kuukashifu mto Nile.

Mwimbaji wa Misri Sherine Abdel Wahab amehukumiwa miezi sita gerezani kwa kutania juu ya hali ya usafi wa mto Nile.

Sherine, ni mmoja wa waimbaji maarufu nchini humo pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice- aliwaambia mashabiki wake kuwa kunywa maji ya mto huo kunaweza kumpatia vijidudu “Kunywa Evian badala yake.” akatania.

Sherine, amehukumiwa na mahakama moja Cairo kwa kusambaza habari zisizo za kweli. Chombo cha habari Misri, Ahram kimesema aliagizwa kulipa paundi 5,000 za Misri.

Mashtaka dhidi ya Sherine yalifunguliwa mwezi Novemba, baada ya kuonekana video mtandaoni ikimuonesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya mto Nile?).akajibu ”Nikinywa maji ya mto Nile nitapata kichocho”. Kichocho ni ugonjwa unaojitokeza maeneo ya vijijini nchini Misri.

Mbali na kesi hiyo mwanamuziki mwengine Shyma ilihukumiwa pia kwa kucheza video yenye kuonesha maadili mabovu

Mwanamuziki Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu
Mwanamuziki Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu
Maamuzi ya mahakama yaliyotolewa siku ya Jumanne inafanya idadi ya wanamuziki kuhukumiwa kifungo kufikia watatu miezi ya hivi karibuni

Mwezi Desemba, Shaimaa Ahmed ajulikanaye kifupi Shyma alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kuonekana kwenye Video ya muziki akiwa amevalia nguo za ndani huku akila ndizi kwa mbwembwe.

alikutwa na hatia ya kuweka video yenye maadili mabaya akahukumiwa sambamba na muongozaji wa video hiyo.Baadae hukumu ilipunguzwa na kuwa ya mwaka mmoja baada ya kukata rufaa.
chanzo: zanzibar24.

Comments