Sami Hafez Anan, mkuu wa zamani wa jeshi la Misri hivi karibuni alitangaza kuwa atachuana na Rais Abdel Fattah el Sisi katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kuwanyika mwezi Machi mwaka huu.
Hata hivyo inaonekana kwamba rais wa Misri hataki kuwa na mpinzani anayehatarisha nafasi yake ndio maana Anan ametiwa mbaroni huku jeshi la nchi hiyo nalo likilaani kitendo chake cha kujitokeza kugombea urais.
Wiki moja baada ya kuwekwa kizuizini Sami Anan ambaye ni mwenyekiti wa chama cha "Misri al Uruba," sasa mwanawe Samir naye ametiwa mbaroni kwa madai ya ubadhirifu.
Mahmoud Raf'at, mratibu wa timu ya uchaguzi ya Sami Anan ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba Samir ametiwa mbaroni kwa ajili ya kusailiwa.
Sami Hafez Anan aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Misri mwaka 2005. Hata hivyo alipoteza cheo hicho baada ya kuingia madarakani Mohammad Morsi, rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri.
Morsi alimteua Jenerali Abdel Fattah el Sisi kuwa mkuu wa jeshi katika juhudi za kuzima uasi wa wanajeshi.
Hata hivyo huyo huyo Jenerali el Sisi ndiye aliyemgeuka Morsi na kuongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyomg'oa madarakani rais huyo wa wananchi mwaka 2013 na kuchukua yeye madarakani ya nchi mwezi Juni 2014.
Comments