Mbunge
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemshambulia kwa
maneno Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina juu ya 'operation'
anazozifanya za kionevu za kupambana na uvuvi haramu kwa kumwambia aache
kufanya kazi kwa mihemuko
Msukuma
ameeleza hayo katika mkutano wa 10 kikao cha sita cha Bunge
kinachoendelea mjini Dodoma wakati akichangia uwasilishaji wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya kilimo, mifugo na maji baada ya kupita miezi kadhaa
tokea Waziri Mpina kutoa kauli yake kuachia madaraka endapo tatizo la
uvuvi haramu litaendelea kuwa sugu nchini jambo ambalo kwa sasa Msukuma
anadai kiongozi huyo analifanya bila ya kufuata sheria zilizopo kwa
kuzuia watu wasivue dagaa na kupelekea kuwapa athari wananchi wanyonge
na kumuomba aundiwe tume ya uchunguzi yeye na timu yake.
"Toka
nazaliwa sijawahi kuona sheria hizi zinazotumiwa na Waziri wa Mifugo
Mpina, umri wangu huu nimeshuhudia awamu zote za Mawaziri.
"Nafikilia kwamba ndio tunaanza kutunga sheria au hii ilikuwa imefichwa ndio inaibuka. Sijawahi kuona Waziri anasimama na kujisifu kwamba kwao hakuna samaki na kutamani watu wote wasile samaki.
"Mungu ametupa neema tofauti, sijawahi kuona mtu anaenda kukamata mitego dakika mbili faini hana unachoma nyavu zake bila ya kuhakikisha kwamba ni feki au laa",alisema Msukuma.

Aidha,
Msukuma amesema ana muhitaji Waziri huyo siku akihudhuria Bunge basi
aweke wazi kuhusiana na sheria hizo anazozitumia amezitoa wapi na kama
akishindwa kutokea katika kipindi basi watamsubiri katika Bunge la
bajeti ili wambane vizuri juu ya hilo.
"Nitoe
rai kwa Mawaziri kwamba Mawaziri wa aina kama hii nina washauri
wapunguze mihemuko kwa sababu hata sisi tunatamani kuendelea kuwa
Wabunge humu ndani lakini kwa 'dizaini' mnayoenda mtuambie mmewapanga
wabunge wa kina nani ambao mnataka wawe wabunge maeneo yetu. Nina
zungumza kwa wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa sidhani kama sisi tutarudi
humu Bungeni", amesisitiza Msukuma.
Kwa upande mwingine, Msukuma amemtaka Waziri Mpina na timu yake kiujumla wajipange kuwafundisha wavuvi na wala sio kuwafilisi.
chanzo:Mpekuzi.
Comments