Mjadala: Wasanii washike siasa au sanaa yao?.

Upo msemo wa Waswahili unaosema kwamba mshika mawili moja humponyoka. Huenda maneno hayo yakawa na ukweli au yasiwe na ukweli ukilinganisha na mifano ambayo tunayo wazi kwenye jamii.
Wapo wasanii walichomoza kwenye siasa na wengine waliingia kwenye siasa na kupotelea huko.
Nyota wa muziki wa Hip Hop miaka ya nyuma walikuwa wakitumia nyimbo zao kufikisha ujumbe wa kisiasa ndani na nje ya nchi zao. Ilifikia hatua muziki huo ukaitwa muziki wa kiharakati.
Wamarekani weusi (Black America), walikuwa wakitumia mashairi yao ya Hip Hop kutetea ubaguzi wa rangi ambao ulikuwa ukifanywa na watu weupe na sauti zao zilikuwa zikisikika kwani hata Martin Luther King (Mshairi), alikuwa akitumia mashairi yake na maongezi kuonyesha kuchukizwa na hali hiyo.
Miaka ya karibuni mambo yaligeuka kidogo. Wasanii wa Hip Hop wameweza kuingia kwenye siasa na kuchukua nafasi mbalimbali. Wengine bado wanapambana lakini hajawajafanikiwa.
Nini maoni yako wasanii waendelee na Sanaa zao au washike siasa kama ambavyo wengine wameamua kujitosa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi.

Comments