Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewasili Jijini Mwanza jana jioni na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo leo mkoani Simiyu.
Katika
ziara hiyo inayoanza leo tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe
22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji
Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na
wanachi Lamadi.
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa katika eneo la Nyaumata.
Miradi
mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa
Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa
Serikali za Mitaa za Mjini.
Makamu
wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia
wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini,
Mwandoya (Meatu)
Tarehe
21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa
Viwanda Tanzania kisha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya
Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jengo la upasuaji la Samia
Suluhu Hassan katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa na kuzungumza na
wananchi katika viwanja vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria.
chanzo:Mpekuzi.
Comments