Leo ni siku ya Alkhamisi 22 Februari, 2018.

Alkhamisi 22 Februari, 2018Leo ni Alkhamisi tarehe 5 Jamadithani 1439 Hijria sawa na 22 Februari, 2018.

Siku kama ya leo miaka12 iliyopita, inayosadifiana na 22 Februari 2006, Haram takatifu ya Maimamu al Hadi na Hassan al-Askari katika mji wa Samarra nchini Iraq, ziliharibiwa vibaya kwenye mashambulizi kadhaa ya miripuko ya mabomu yaliyofanywa na makundi ya kigaidi na kupelekea hasara kubwa za mali na watu. 
Maimamu hao ni wajukuu wa Mtume Bwana Mtume Muhammad SAW, na waliokuwa na nafasi kubwa ya kielimu na uchaji-Mungu katika zama zao. 
Kitendo cha kuharibiwa eneo hilo kiliwakasirisha mno Waislamu duniani hususan wafuasi wa Ahlul Bait wa Mtume (saw). 
Nukta ya kufaa kukumbusha ni kwamba, kabla ya kujiri mashambulizi hayo, ulinzi wa haramu hizo, ulikuwa kwa majeshi vamizi ya Marekani. 
Shambulio hilo lilifanyika kwa lengo la kuzusha ufa kati ya safu za Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni nchini Iraq.
Katika siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, wapiganaji shupavu wa Iran walianzisha operesheni ya 'Khaybar' dhidi ya majeshi ya Iraq, kwenye vita vya kulazimishwa vilivyoazishwa na utawala wa Baath wa Saddam Hussein. 
Katika operesheni hiyo iliyofanyika katika eneo la Hoor al Hoveyzeh kusini magharibi mwa Iran, wapiganaji shupavu wa Iran walifanikiwa kuvuka maji na kukiteka kisiwa chenye utajiri mkubwa wa mafuta cha Majnoon, kilichoko karibu na mji wa Basra kusini mashariki mwa Iraq.
Miaka 60 iliyopita katika siku kama ya leo yaani tarehe 22 Februari mwaka 1958, Abul Kalam Ahmad Azad, msomi, khatibu na mwanasiasa wa India alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 70. 
Abul Kalam Azad alianza harakati za kisiasa akiwa na umri wa miaka 17 na harakati zake zilikuwa  dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza kwa shabaha ya kuwazindua Waislamu wa India. 
Msomi huyo alifungwa gerezani mara kadhaa na wakoloni wa Kiingereza, kutokana na hatua zake za kuchapisha na kutoa hotuba zilikuwa zikifichua ukandamizaji wa Uingereza. 
Mara baada ya India kupata huru, alichaguliwa kuwa mbunge na Waziri wa Elimu na Malezi wa nchi hiyo.
Na miaka 767 iliyopita katika siku kama ya leo sawa na tarehe 5 Jamadithani mwaka 672 alifariki dunia Jalaluddin Muhammad Balkhi maarufu kwa jina la Maulawi, mshairi mkubwa wa Iran katika mji wa Kunya ambao ni moja kati ya miji ya zamani ya Iran ulioko kusini mwa Uturuki ya leo. 
Maulawi alihesabiwa kuwa mshairi mkubwa na maarufu zaidi katika karne ya 9 Hijria Shamsia na miongoni mwa wanafikra na wachamungu wakubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. 
Maulawi alizaliwa mwaka 604 Hijria Shamsia katika mji wa Balkhi kaskazini mwa Afghanistan ya sasa na baada ya muda akahamia katika mji wa Konya akiandamana na baba yake. 
Baadaye alielekea Syria kwa ajili ya masomo ya juu. 
Miongoni mwa vitabu muhimu zaidi vya Maulawi ni Mathnawi Maanawi, Fihi ma Fihi, Maktubat Maualana na Rubaiyyat.
 Hii ni kwa hisani ya parstoday.

Comments