Kuongezeka matatizo ndani ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani.

Kuongezeka matatizo ndani ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani Mwanadiplomasia mmoja wa zamani wa Marekani amesema kuwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo hivi sasa inakabiliwa na matatizo chungu nzima.

Elliot Abrams aliyekuwa katibu wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani wakati wa utawala wa Rais Ronald Reagan ameeleza kuwa wanadiplomasia zaidi ya 100 wameondoka katika Wizara hiyo ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani wakati huu ambapo Rex Tillerson anaongoza wizara hiyo. 
Katibu huyo wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wakati wa utawala wa Rais Reagan amesisitiza kuwa wizara hiyo ya Marekani hivi sasa inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi. 
Elliot Abrams ameongeza kuwa asilimia 30 ya nyadhifa za mabalozi katika balozi za Marekani katika baadhi ya nchi duniani zikiwemo Saudi Arabia, Jordan, Misri, Ujerumani, Austria, Korea ya Kusini na katika nchi nyingine za Amerika ya Latini hivi sasa zipo wazi. 
Katibu huyo wa zamani wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amebainisha kuwa hatua ya kuwa wazi asilimia zaidi ya 30 ya nyadhifa za mabalozi katika balozi za Marekani katika pembe mbalimbali duniani ni kosa kubwa lililofanywa na Rais wa sasa Donald Trump na Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni Rex Tillerson. 
Ripoti zinaonyesha kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani anahitilafiana kimtazamo na watu wa karibu na Trump akiwemo Jared Kushner mkwe wa Rais huyo wa Marekani kutokana na kuingilia masuala ya wizara hiyo.  
chanzo:parstoday.

Comments