Mbunge
wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea amevitaka vikundi vinavyodaiwa kuwa vya
CCM vinavyozunguka kuandikisha vitambulisho vya watu kuacha mara moja
kabla hawajachukua hatua ambazo amezitaka zisilaumiwe.
Akizungumza
jana na wanahabari, Kubenea alisema kwamba wamegundua wapo vijana ambao
wamekuwa wakilizunguka jimbo la Kinondoni na kuwalaghai wapiga kura kwa
kununua vitambulisho, kuchukua shahada pamoja na kununua vitambulisho
hivyo ili kupunguza idadi za wapiga kura kwa makusudi.
Kubenea
amesema kwamba endapo vikundi hivyo vitakaidi agizo hilo
watashughulikiwa kama wahalifu kwani kitend wanachokifanya ni kitendo
cha uhalifu.
"Mnyika
alituambia kuwa wanaofanya hivyo ni vibaka kama vibaka wengine, hivyo
wanapaswa kushughulikiwa. Na sisi tunasema kwamba Tutaingiza vijana
wetu mitaani ili washughulikiwe na lolote litakalotokea wasituulize."
Kubenea
Pamoja na hayo kubenea amesema kwamba tayari wamekwishapeleka malalamiko yao katika vyombo husika.
Kubenea
kwa sasa ndiye Kampeni Meneja wa Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Salum
Mwalimu wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa
kufanyika Februari 17
chanzo:Mpekuzi.
Comments