Kapombe, Kazimoto nyota pekee walioshudia kipigo cha Libolo.

Baada ya miaka mitano Simba imerejea katika mashindano ya kimataifa kwa kishindo baada ya kuichapa Gendarmerie ya Djibouti kwa mabao 4-0 katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo uliofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kama Simba ikipata ushindi wa jumla katika mchezo huo basi itakutana na mshindi kati ya El Masry ya Misri na Green Bufaloes ya Zambia katika hatua itakayofuata.
Simba imerejea katika mashindano ya kimataifa baada ya miaka mitano kupita tangu walipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2013.
Kocha Mserbia Milovan Cirkovic ndiye wa mwisho kuiongoza Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2011/2012 na kukata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hata hivyo, kocha huyo baadae aliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mfaransa Patrick Liewig ambaye aliingoza Simba kwenye mashindano ya kimataifa mwaka 2013 na kutolewa raundi ya kwanza tu na Recreativo de Libolo ya Angola.
Simba ilitolewa  katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 5-0 na Recreativo de Libolo ya Angola, ikifungwa 1-0 nyumbani jijini Dar es Salaam na mabao 4-0 ugenini.
Hiki ni kikosi cha Simba ambacho mara ya mwisho kilishiriki mashindano hayo na sasa wapo wamebaki wachezaji wawili tu ambao watashiriki tena mashindano hayo mwaka huu.
Juma Kaseja- Ndio alikuwa kipa namba  moja wa Simba amabye alidaka katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam  lakini ugenini akapigwa benchi.Hivi sasa anaichezea Kagera Sugar.
Abel Dhaira - Kipa mwingine ambaye naye alikuwemo katika kikosi cha Simba mabacho mara ya mwisho kilishiriki mashindano ya kimataifa.Alipewa nafasi kwenye mchezo wa marudiano uliofanyika nchini Angola na kupigwa mabao manne. Hivi sasa ni marehemu.
Nassor Masoud'Chollo'- Naye alikuwemo katika kikosi hicho akicheza mechi zote mbili ya Dar es Salaam na Angola. Hivi sasa anaichezea Dodoma FC ambayo hata hivyo  imeshindwa kupanda daraja kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Shomari Kapombe - Alicheza michezo yote miwili nyumbani na ugenini. aliwahi kutimkia Ufaransa kucheza soka la kulipwa kabla ya kurejea na kujiunga na Azam hata hivyo sasa amerejea katika kikosi hicho na atashiriki tena katika mashindano ya kimataifa mwaka huu.
Juma Nyoso - Naye ni mmoja wa wachezaji waliokuwemo katika kikosi cha mwisho cha Simba kilichosriki kimataifa. Hivi sasa anaichezea Kagera Sugar.
Komabil Keita - Beki raia wa Mali ambaye naye alikuwemo katika kikosi hicho, lakini baadae aliondolewa kwa madai ya kushuka kiwango.
Amri Kiemba - Mmoja wa wachezaji walioichezea Simba mashindano ya kimataifa mwaka 2013.Hivi sasa ameamua kustaafu soka.
Mrisho Ngassa - Anaichezea Ndanda hivi sasa kwenye Ligi Kuu Bara, lakini naye alikuwemo katika kikosi cha mwisho cha Simba kilichoshiriki mashindano ya kimataifa miaka mitano iliyopita.
Haruna Chanongo- Naye alikuwepo katika kikosi cha Simba, lakini sasa anaichezea Mtibwa Sugar.
Salim Kinje- Alitimikia Kenya na kujiunga na AFC Leopards kwa sasa amestaafu soka.
Haruna Moshi 'Boban' - Alikuwepo katika kikosi cha Simba mwaka 2013,hivi sasa naichezea Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Mwinyi Kazimoto- Miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi dhidi ya Libolo baada ya hapo alitimikia uarabuni kucheza soka la kulipwa kabla ya kurejea na kujiunga tena na Simba.
Abdallah Seseme- Huyo ni miongoni mwa chipukizi waliokuwa katika kikosi cha Simba kilichoshiriki mashindano ya kimataifa kwa sasa yupo Mwadui.
Felix Sunzu- Mshambuliaji Mzambia alijijengea jina kubwa kwa uwezo wake wa kuzifumani nyavu alichezea Simba katika mechi dhidi ya Libolo kwa sasa yuko Zambia.
Kiggi Makasi- Baada ya kuichezea Simba aliandamwa na majeruhi yaliyotishia kuua kibaji chake, lakini kwa sasa amerudi katika ubora wake na Singida United.


Ramadhani Chombo ‘Redondo'- Kiungo mwenye ubunifu wa hali ya juu alikuwepo katika kikosi cha Simba kulichochapwa bao 5-0 na Libolo kwa sasa ni mchezaji Friends Rangers.

Comments