Aidha gazeti hilo sambamba na kukosoa matamshi ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala huo ambaye alisema kuwa, hatua ya kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda mji wa Quds, itailetea furaha na sherehe Israel, limeandika kuwa, kwa kuzingatia matukio hasi yatakayofuatia hatua hiyo hususan katika kadhia ya utatuzi wa mgogoro kati ya Israel na Wapalestina, sula hilo halitakuwa na maslahi kwa Tel Aviv.
Aidha gazeti hilo limekosoa matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekani juu ya kadhia ya amani ya eneo la Mashariki ya Kati kwa kuandika, katika hali ambayo hadi sasa hakushuhudiwi amani yoyote katika eneo, ni vipi itawezekana kuharakisha hatua ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kwenda Quds na kudai kuwa suala hilo litasaidia kuleta amani?.
Hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza azma ya nchi hiyo kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv, mji mkuu wa utawala haramu wa Israel kwenda mji wa Quds, hatua ambayo imetajwa na walimwengu kuwa inalenga kuibua ghasia na machafuko zaidi eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, uhamishaji huo wa ubalozi utafanyika tarehe 14 Mei mwaka huu, ambayo inasadifiana na siku ya Nakba, inayokumbushia tukio la kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina na utawala katili wa Kizayuni.
chanzo:parstoday.
Comments