Chungu chenye maandishi ya kiarabu chafukuliwa katikati ya kiwanja champira Kigunda Unguja.

Imani ya kishirikina iliojitokeza katika kiwanja champira cha nyayo huko Kigunda Wilaya ya Kaskazini A Unguja na kuwawekea wakati mgumu viongozi wa chama hicho baada ya kujitokeza watu wasiojitokana kukizika kijungu kikiwa na maandishi ya kiarabu ambayo yameandikwa kwa damu hali ambayo iliyo waletea hofu katika eneo hilo.

Mmmoja miongoni mwa viongozi wa kiwacha hicho Ali Khamisi anasema kuwa alipopata ripoti kutoka kwa wachezaji wake kuwa kunabaadhi ya watu wamekuja kufanya ushirikina walishirikiana kwapamoja kukitafuta kijungu hicho na tayari wameshafanikiwa kukiona na ndani yaki kimeandikwa baadhi ya majina baadhi ya wachezaji.

Hata hivyo viongozimwa kiwanja hicho wamewashauri viongozi wa Serikali kuwasaidia katika kuandamana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika kiwanja hicho ili fani yao yamichezo iweze kuendelea.

Nae Sheha wa Shehia ya Kigunda Makame Madina amethibitisha nkuwepo kwa kitendo hicho.

“hili tukio kweli limetokea na linaonesha wazi kuwa limetendeka kwa imani za kishirikina kimeoneka kijungu kikiwa kina maandishi yakiarabu nahuyo aliefanya kitendo hicho tuna mjua na kwani aliendakuazima mtaimbo sehemu akaonekana kwahiyo tunamtaka aje ajisalimishe mwenyewe  na kama hajajitokeza tutamfichua”

Comments