Akihutubia katika mkutano wa usalama wa Munich Ujerumani hapo jana Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel huku akiwa amebeba kile alichokitaja kama pande la mabaki ya ndege isiyo na rubani ya Iran aliyodai eti imetunguliwa na jeshi la Israel zaidi ya wiki moja iliyopita, alidai kuwa Tel Aviv ina uwezo wa kutoa jibu la moja kwa moja dhidi ya Iran.
Brigedia Jenerali Salami amesema kuwa, hatua ya maonyesho na mchezo wa kuigiza ya viongozi wa Marekkani na utawala haramu wa Israel inaonyesha kuwa, nafasi na daraja yao imeshuka na wanakabiliwa na mazingira magumu katika kukabiliana na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Kwa upande wake, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamun ya Iran ameyataja matamshi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika kikao hicho kama mchezo wa kuigiza wa katuni, ambayo hayana hata thamani ya kujibiwa.
Itakumbwa kuwa, Zarif alisema katika hotuba yake katika mkutano huo wa usalama wa Munich Ujerumani kwamba, ni jambo la kushangaza kuona Marekani na waitifaki wake wanaielekezea kidole cha lawama Iran, katika hali ambayo Jamhuri ya Kiislamu imekuwa katika upande mzuri wa historia kwa kukabiliana na dikteta Saddam Hussein, makundi ya kigaidi ya al-Qaeda, Taliban, Daesh, Jabhatun Nusra na mfano wake.
Comments