
Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya kuandika
habari za kiuchmi mkoani Mtwara meneja wa kitengo kinachosimamia fedha
za kigeni kutoka benki kuu ya Tanzania Eliyamringi Mandari amesema
kufungwa kwa maduka hayo kunatokana na oparesheni inayoendelea nchi
nzima kwa sasa yenye lengo la kuleta ufanisi wa kazi katika maduka hayo.
Amesema upareresheni hiyo inakwenda sambamba na usajili upya wa
maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo imetokana na kanuni
mpya ya kusimamia maduka hayo lengo hasa ni kuongeza ufanisi na mitaji
katika kuendesha biashara hiyo.
Hata hivyo amesema katika oparasheni hiyo maduka 297 yametuma maombi
yao huku maduka sitini na tano yanaendelea kufanyiwa kazi, sabini na
moja tayari yamepatiwa leseni mpya pamoja na matawi yake arobaini.
Amesema maduka 86 yamefutiwa leseni kutokana na kushindwa kutimiza
masharti ikiwemo kueleza vyanzo vya mitaji inayotumika katika kuendesha.
Biashara hiyo na kusisitiza wiki mbili zijazo zoezi hilo litakamilika na taarifa kamili itatolewa.
Kufuatia opareheni hiyo mandari amesema ni kosa la jinai kwa mtu
yeyote kuendesha biashara ya fedha za kigeni bila leseni ya benki kuu
adhabu yake ni faini shilingi milioni nne, ama kifungo cha miaka kumi na
nne gerezani, ama vyote viwili.
Source: ITV
Comments