
Tukio hilo limetokea huko kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja.
Ambae ni Bibi wa Mtoto huyo amesema majira ya saa 5 usiku amegongewa mlango na kuletewa mtoto huyo akiwa na majeraha.”
“Alikuja Sheha Mstaafu kuniamsha na mumewangu usiku akanambia tumekuletea mtoto ili umuharakize hospitali kupata matibabu kapigwa panga, kumfunua mtoto na kumtizama apoapo tulianza kulizana pamoja na majiani Uyomfanya tukio kafanya mbali na baadae akaja kwangu akaanna kunitukana na neno lake la mwisho alilolizungumza kuwa baina yangu na mwanangu na alie mkata panga atatukata vichwa naavitie kwenye polo akavipeleke Polisi”
“ mimi ikanibidi nifunge mlango kwakuogopa Mumewangu akachupa ukuta akatokezea nje nailikua anajisu mkononi anarandanalo”
“Wallahi kamkata mguu mtoto wa miezi mitano halafu akachukua kisu akapaperekecha na akamrembea msituni ukimuona huyo mtoto utatokwa na machozi na sasaivi yupo spitali ya makunduchi kalazwa”alisema bibi wa mtoto huyo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Makarani Khamis Ahmed amesema tuna mshikilia muhalifu aliethubutu kumjeruhi mtoto wa miezi mitano kwa kumpiga panga na mguu wa kushot pasi na hatia yoyote.
Hadi sasa muhalifu huyo tayari ameshawekwa mikononi mwa Polisi na mtoto anaendelea na matibabu.
Comments