Serikali
ya Kenya imemfukuza kwa nguvu na kumsafirisha kwenda nchini Canada
mmoja wa viongozi wa upinzani Kenya, Miguna Miguna usiku wa kuamkia leo
Februari 8 baada ya mahakama kudai aachiwe huru.
Katika
akaunti ya Twitter ya Serikali inayofahamika kwa jina la ‘Nexus’
iliandika katika ukurasa huo Februari, 6 saa 7:19 usiku kuwa Miguna
anaelekea nyumbani Canada baada ya mahakama kuamuru aachiwe.
Serikali
imeandika kuwa Wizara ya Ulinzi ilitii agizo hilo na kumpatia tiketi ya
kwenda nyumbani kwake Canada ambapo ana uraia wa nchi hiyo alioupata
Juni 16, 2017.
“Miguna
ameelekea nyumbani. Mahamakma iliamuru aachiwe na Wizara ya Ulinzi
imetii amri na imempatia tiketi ya kwenda nyumbani. Tafadhali
tunasisitiza alipatiwa kibali cha kuishi Canada Juni, 16 2017” umeandika ukurasa huo.
Miguna
amesafirishwa na Shirika la Ndege la KLM ambalo lilipoulizwa na
wananchi katika ukurasa wao wa Twitter unaofahamika kwa jina la ‘Royal
Dutch Airline’ walipendekeza maswali yote waulizwe mamlaka husika kwa
sababu za kiusalama.
Miguna
alishikiliwa na Polisi Februari, 2 kwa tuhuma za kushiriki kuapishwa
kwa Raila Odinga kama Rais wa watu wa Kenya Januari, 30.
Mwanasheria wa Miguna, Dk John Khaminwa amesema mteja wake kwasasa hayupo nchini humo.
“Ni kweli. Ameondolewa kwa nguvu na ndege ya KLM na tunasikia ameelekea Canada. Ni uvunjaji wa haki” amesema Khaminwa.
Kuhusu
sakata la uraia wake, Dk Khaminwa amesema Miguna aliukana uraia wa
Kenya ila miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu aliomba tena.
“Miguna alipokamatwa Serikali ya Canada iliiandikia barua Kenya kuelezea kuwa mwananchi wao ananyanyaswa,” amesema Khaminwa.
Katika
kipande kifupi cha video kinachosambaa mtandaoni kimemuonyesha kiongozi
huyo akiwa katika ndege na amevalia suti, barakashia akiwa peke yake
siti za mbele.
Comments