Mbunge
wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe,
ameuzungumzia mwaka 2017 huku akiukaribisha mwaka mpya 2018, kwa kusema
kuwa tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu lilimgharimu.
==>Hapo chini ni ujumbe wa Zitto Kabwe
Tunawatakia
heri ya mwaka mpya 2018. Mwaka 2017 ulikuwa na changamoto lukuki lakini
pia mafanikio makubwa kwetu kama chama. Mkutano wa miaka 50 ya Azimio
la Arusha jijini Arusha ilikuwa mafanikio ya juu kiitikadi. Kwangu Mimi
Hotuba ya Arusha ilikuwa bora kimaudhui na ilipaswa tutoe kitabu cha
Hotuba ile.
Mkutano
Mkuu wa Kidemokrasia Jijini Mwanza kuhusu Maendeleo bila kupoka Uhuru
wa watu ulitusaidia kuweka msimamo wetu kuhusu ubinywaji wa haki na
Uhuru unaoendelea nchini.
Tukio
la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na
lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia.
Ilinigarimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani
tukio lile. Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua
Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema
zaidi.
Kuondoka
wanachama waandamizi ilikuwa pigo. Pigo hili limetupa funzo kubwa Sana
na hivyo Tutaendelea kuwepo na imara zaidi mwaka 2018.
Chama chetu kinawatakia heri ya mwaka 2018. Tunamshukuru Mungu kwa mwaka 2017
chanzo:Mpekuziblog.
Comments