Zarif: Uhai wa JCPOA unategemea kufungumana kikamilifu US.

Zarif: Uhai wa JCPOA unategemea kufungumana kikamilifu USWaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran haitaendelea kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, iwapo Marekani itayakiuka.

Mohammad Javad Zarif aliyasema hayo jana kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter mjini Moscow hapo jana ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake Sergei Lavrov, kabla ya kuelekea Brussels kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Zarif amesema, na hapa tunanukuu: "Sote tunakubaliana kuwa, ni muhimu kwa pande zote za makubaliano hayo ya Vienna kuheshimu na kufungamana kikamilifu na mapatano hayo. Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, mara kadhaa umethibitisha kuwa Iran imetekeleza wajibu wake, lakini kuendelea kwake kufungamana na JCPOA kutategemea na kufungamana kwa Marekani."
Mwezi wa Oktoba mwaka jana, Rais Donald Trump wa Marekani alikataa kuidhinisha kufungamana Iran na mapatano ya JCPOA yaliyofikiwa mwaka 2015 baina ya Iran na madola sita makubwa duniani ambayo ni Marekani yenyewe, Ufaransa, Uingereza, Russia, China na Ujerumani.
Iran imesisitiza kuwa maadamu wote waliofikia mapatano ya JCPOA wanafungamana nayo, basi itaendelea kufungamana na mapatnao hayo ya nyuklia lakini iwapo Marekani itajiondoa katika Mapatano hayo, Iran nayo itachukua hatua mkabala wake.
 chanzo:parstoday

Comments