
Akitoa taarifa hiyo mkuu wa
kitengo cha maliasili zisizorejesheka Ngwali
Makame haji amesema mchanga huo umekamatwa katika eneo la kianga na mwera
uliochimbwa kutoka kambi ya jeshi welezo.
Aidha amesema mwezi Disemba mwaka
jana pia walikamata shehena 200 za
mchanga katika maeneo ya Uzi wilaya ya
kusini ambapo ulichimbwa katika mashamba
ya kilimo na pembezoni mwa bahari.
Kutokana na hali hiyo amesema
wameandaa kikao maalum ili kuondosha suala la uchimbaji wa mchanga kiholela kwa
kupita kila wilaya ili kuzungumza na
wanaojishughulisha na shughuli hizo.
Sambamba na hayo amewataka
wananchi na masheha kutoa taarifa ili kudhibiti uchimbaji wa mchanga katika
maeneo yasiyoruhusiwa.
Comments