Lebo
ya muziki ya WCB jana usiku ilitambulisha msanii mwingine ambaye kazi
zake zitakuwa zikisimamiwa na lebo hiyo, ambapo mbali na kumtambulisha,
msanii huyo aliachia ngoma yake ya kwanza akiwa chini ya WCB.
Msanii
huyo ni Mbosso ambapo awali alikuwa mmoja kati ya wasanii wanne
waliokuwa wakiunda kundi la Ya Moto Band ambalo limesambaratika.
Kabla ya kujiunga na WCB, Mbosso alikuwa akitumia jina la Marombosso.
Hapa chini ni video yake mpya aliyoiachia jana mara baada ya kutambulishwa.
chanzo:Mpekuzi.
Comments