Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Myanmar ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa Serikali ya nchi hiyo amepongeza mauaji yanayofanyika dhidi ya Waislamu wa Rohingya nchini humo.
Akiwa katika mkutano wa waandishi habari pamoja na Taro Kono, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Aung San Suu Kyi amepongeza hatua ya jeshi la Myanmar ya kukiri kufanya jinai ya kuwaua Waislamu wa Rohingya na kuitaja kuwa ni hatua chanya! San Suu Kyi amekuwa akitetea na kuhalalisha mauaji yanayoendelea kufanywa na jeshi na Mabudha wa Myanmar dhidi ya Waislamu nchini humo.
Uungaji mkono wa Aung San Suu Kyi kwa mauaji Waislamu wa Rohingya umekosolewa sana na jamii ya kimataifa na jumuia za kutetea haki za binadamu.
Uungaji mkono huo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Myanmar una maana kwamba, mabudha wamefanikiwa kuangamiza kizazi cha Waislamu katika jimbo la Rakhine la Waislamu wa Rohingya na kutwaa ardhi na milki zao na kwamba jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kukamilisha majukumu na kazi yake.
Hii ina maana kwamba, operesheni ya kuwaangamiza na kuwafukuza Waislamu wa Rohingya katika ardhi ya mababu zao imefanyika kwa mpango maalumu uliosimamiwa na kutekelezwa na serikali, Mabudha wenye misimamo mikali ya jeshi la nchi hiyo.
Aung San Suu Kyi pia anatetea kwa fahari mauaji ya Waislamu wa Rohingya kwa sababu amefanikiwa kupata ridhaa na uungaji mkono wa Mabudha. Hii ni licha ya kuwa, jamii ya kimataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yalitarajia kwamba, San Suu Kyi aliyetunukiwa tuzo ya amani na Nobel angechukua hatua za kuzuia mauaji yanayofanywa na Mabudha dhidi ya Waislamu au kwa uchache kulaani jinai na mauaji hayo.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa London nchini Uingereza, Riyadh Kariim anasema: Maangamizi ya kizazi yanayofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya ni ukatili mkubwa unaofanana na mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Waserbia dhidi ya Waislamu wa Bosnia huko Srebrenica. Mauaji hayo ya Myanmar yana vielelezo na sifa zote za mauaji ya umati na ya kimbari kama yale la Srebrenica. Kwa hakika mateso waliyopewa Waislamu wa Rohingya ni ukatili unafanywa na makatili wakifurahia unyama huo (sadism).
Hata hivyo jambo linaloshangaza zaidi ni kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.
Hii ni pamoja na kuwa jamii ya kimataifa inakiri kwamba kunafanyika mauaji ya kimbari nchini humo lakini hadi sasa hakuna hatua yoyote ya maana iliyochukuliwa kusitisha ukatili huo. Msimamo huu wa jamii ya kimataifa ndio uliomshajiisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Myanmar kutetea kwa fahari mauaji ya kimbari yanayofanyika nchini humo.
Kwa vyovyote vile, inatarajiwa kwamba, jamii ya kimataifa itatekeleza majukumu yake ya kibinadamu walau kwa kuchelewa na kuchukua hatua za maana za kusitisha mauaji ya kimbari yanayofanyika Myanmar.
Vilevile hapana shaka kuwa, iwapo duru ya kimataifa zitaishinikiza serikali ya nchi hiyo na kutaka kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya Waislamu wa Rohingya, dunia itashuhudia makaburi mengi ya umati yaliyojaa maiti za Waislamu hususan katika jimbo la Rakhine lililoko magharibi mwa Myanmar.
Suala hili linaweza kuifedhehesha zaidi serikali ya Mabudha wa nchi hiyo na kupaza zaidi sauti ya kutaka kutekelezwa haki na adilifu na hatimaye kuchukuiliwa hatua za kisheria wahusika wote wa mauaji hayo.
chanzo:parstoday.
Comments