Waumini wa kiislamu watakiwa kufuata mwenendo wa Mtume.

Waumini wa dini ya kiislamu nchini wametakiwa kufuata mafunzo na maagizo ya Mtume Muhamad (S.A.W) ili kuweza kupata ujira mwema mbele ya Allah (S.W).
Akitoa wito huo Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuber wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya Maulidi iliyoandaliwa na Kiwanda cha NIDA textile Mills|(T) ltd NAMERA GROUP OF INDUSTIES,  ambapo amewataka Waumini wa dini hiyo kusikiliza na kufuata kile anachokisema Mtume.
“Nitoe wito kwa Waumini wa dini ya Kiislamu kufuata na kusikiliza kile anachokisema Mtume kwa sababu Mtume amefundisha mambo mbalimbali ambayo yana Maslaha kwa binadamu na ulimwengu wao,” Alisema Mufti Abubakar
Kwa upande wake  Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum ambaye alizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi pamoja na uongozi mzima wa kiwanda cha NIDA amesema hafla hiyo inafanyika kila mwaka na kwamba katika kufanya hivi kunasaidia amani ya nchi kuendelea kupatikana kwani katika kuadhimisha Maulidi hayo wanafanya maombi hasa ya kuliombea taifa.

Aidha amewashukuru uongozi wa NIDA pamoja na kuwapongeza kuweza  kuaanda Maulidi hayo kwani kwa kufanya hivyo wanawakumbusha waumini pamoja na watu wa dini zote kutenda mambo mazuri kwa kutegemea ujira mwema mbele ya allah (s.w)
Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali Mgeni rasmi akiwa ni Mh. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, alieambatana na Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohammed Gharib Bilali na Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam .

chanzo: zanzibar24.

Comments