
Kumi kati ya wale waliouwa walikuwa ni raia wa Marekani akiwemo rubani raia wa Costa Rica na rubani msaidizi.
Vyombo vya habari vilisema kuwa watano kati ya wale waliouawa walitoka familia moja.
Ripoti
zinasema kuwa ndege hiyo ya injini moja ya Cessna 208 Caravan, ilikuwa
safarini kutoka mji mkuu San José kwenda Punta Islita ambalo ni eneo
la kistarehe.
Hukukuwa na manusura na wala haibainiki ni nini kilisababisha ajali hiyo.
Kisa hicho kilitokea katika eneo la milima karibu na Bejuco mkoa wa Guanacaste
Rais
wa Costa Rica alithibitisha ajali hiyo katika taarifa iliyochapishwa
mitandaoni akisema kuwa serikali yake imesikitishwa sana na vifo hivyo.
Mtangulizi
wake rais wa zamani Laura Chinchilla, aliandika katika mtandao wa
Twitter kuwa mmoja wa wahudumuwa marubani alikuwa na binamu wake.
chanzo:Bbc.
Comments