Gazeti hilo linalochapishwa mjini
London, Uingereza limewanukuu maafisa wa ngazi ya juu serikalini nchini
Saudia wakisema kuwa, kati ya wanawafalme ambao wanaendelea kushikiliwa
ni pamoja na Al-Waleed bin Talal na Turky bin Abdullah bin Abdulaziz Al
Saud kiongozi mkuu wa zamani wa mji wa Riyadh pamoja na viongozi wa
zamani wa serikali ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wanawafalme
hao wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za utawala huo baada ya
kukataa amri ya kuigawia serikali ya Saudia fedha zao.
Hayo
yanajiri katika hali ambayo Jumamosi iliyopita, wanamfalme wengine 11
walitiwa mbaroni na kupelekwa jela ya al-Ha'ir baada ya kufanya
maandamano mbele ya kasri la Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud
wakilalamikia hatua ya serikali kuwakatia ruzuku ya malipo ya maji,
umeme na marupurupu mengine.
Wakati huo huo, mtandao wa habari wa
al-Ahd wa nchini Lebanon umefichua habari ya kujiri mapigano ya silaha
kati ya wanawafalme watatu na walinzi saba wa jela ya al-Ha'ir ambayo
yamepelekea wanawafalme hao kuuawa kusini mwa mji wa Riyadh.
Tangu
alipochukua hatamu za uongozi Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha
Ufalme na Waziri wa Ulinzi wa Saudia, amekuwa akitekeleza siasa za
kuwashusha hadhi wanawafalme wengine ili kwa njia hiyo aweze kuvunja
kambi ya upinzani dhidi yake.
chanzo: parstoday.
Comments