
Mhe khatibu ameyasema hayo wakati akishiriki katika kazi za usafi wa
pembezoni mwa barabara ya kitogani hadi paje kwa wanachama wa pressure
group meli nne taveta kinajijitolea kufanya kazi za usafi katika maeneo
mbali mbali hapa nchini.
Amesema Serikali itaendelea na wajibu wake wa kuimarisha huduma
muhimu za kijamii ikiwemo miundo mbinu ya barabara lakini jukumu la
kuitunza litabaki kwa kila mwananchi hivyo ni vyema wakaunga mkono
juhudi hizo ili ziendelee kuleta manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla .
Amefahamisha kwamba uwekaji wa barabara katika hali ya usafi ni njia
moja wapo ya kivutio cha wageni wanaoingia nchini jambo ambalo
linasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya utalii ambayo ni tegemeo
kubwa katika kukuza uchumi.
Nao wanachama wa kikundi hicho wamesema wataendelea na juhudi zao za
kujitolea katika shughuli za kuweka usafi katika maeneo mbali mbali
mjini na vijjini.
Nae msimamizi wa njia wilaya ya kusini bwana Kussein Omar Hussein
amewashukuru wana kikundi hao kwa jitihada zao walizozionyesha na
kuwataka kuwa waangalifu wakati wanapofanya usafi pembezoni mwa barabara
ili kuepukana kupasua mambomba ya maji yaliopita katika maeneo hayo.
chanzo: zanzibar24.
Comments