Shirika la Habari la Associated Press limetangaza kuwa, matokeo ya ripoti hiyo iliyosambazwa Alkhamisi ya jana na 'Kamisheni ya Sheria za Kiraia nchini Marekani' yanaonyesha kwamba, wanafunzi wanaotoka familia za kipato cha chini za Wamarekani weusi na malatino kwa kawaida wanasoma katika mazingira magumu sana ndani ya shule za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanafunzi weusi na wale wa malatino wanalazimika hata kutumia vitabu vya zamani huku walimu nao wakijizuia kuwapa umuhimu wowote.
Katika ripoti hiyo imeelezwa kwamba, kukosekana usawa huko kumewafanya mamilioni ya wanafunzi wanaosoma katika shule za serikali kusoma katika hali ngumu na kunyimwa haki, suala ambalo linawafanya aghlabu yao kuwa na vinyongo.
chanzo:parstoday.
Comments