Wakulima waendelea kulalamikia uharibu wa kilimo chao Unguja.

Related imageLicha  ya  jitihada  zinazochukuwa  na jeshi la polisi katika   kudhibiti  uingizwaji  wa  wanyama  katika  mashamba ya wakulima  lakini  bado  baadhi  ya  wafugaji  wanaendelea  na  vitendo  hivyo  jambo ambalo hurejasha  nyuma  maendeleo  ya wakulima.

Hayo yamebainishwa  na baadhi ya wakulima kufuatia  kukithiri  kwa  vitendo  hivyo  katika  shehia  ya  kiboje  mkwajuni    wamesema  wanajishughulisha  na  shughuli za kilimo  kwa lengo  la  kujikwamuwa   kimaisha  lakini  bado wanakabiliwa  na  tatizo  la uingizwaji wa wanyama  katika  mashamba.

Nae  MABROK JUMA  KHAMIS  ambae ni  sheha  wa  shehia  hiyo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na  amesema   jitihahada nyingi  zinachukuliwa  na  jeshi  la polisi  katika  kuondowa  vitendo  hivyo  lakini  bado  baadhi  ya  wafugaji  hawathamini  nguvu  za  wakulima.


Hata  hivyo  amewataka  wakulima  na  wafugaji  kuwa na mashirikiano  ya  pamoja  katika  kuendeleza   shughuli  za  uchumi  kwa  lengo  la  kujikwamuwa  na  hali  ngumu  ya  maisha.

Comments