Waislam watakiwa kuendelea kujitolea kwa ajili ya ujenzi Kidoti Unguja.

Related image
Waislamu wametakiwa kuunganisha nguvu zao kwa pamoja kwa lengo la kukamilisha ujenzi wa mskiti mkuu wa kidoti.

Akizungumza na Assalamu fm katibu  mkuu wa ijitimai Zanzibar Amir Hafidh Jabu amesema waislamu ni vyema kushiriki   kwa hali na mali  ili kupeleka mbele harakati za dini ya kiislamu.

Aidha amesema kina mama wameonekana kujitokeza kwa  wingi  katika kuunga mkono ujenzi  huo.

Kwa upande wao kina mama  hao  wamesema wanafanya  juhudi ili kuhakikisha ujenzi unakamilika ikiwa ni pamoja na  kujishughulisha katika  kilimo ili kusaidia fedha kwa ajili ya msikiti huo.


Mskiti mkuu wa kidoti wenye uwezo wa kuchukua  waumini  5100 unatarajiwa kuezekwa baada ya miezi mitatu na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili na milioni mia nane hadi kumalizika kwake. 

Comments