Waislam wakumbushwa kuendelea kuisoma QURAN.

Image result for smzNa Mohd Nassor.
Waislam nchi washauriwa kupenda kukisoma kitabu kitakatifu cha Quran kwani ndio msingi wa maisha  bora ya mwanandamu hapa duniani na kesho akhera.

Ushauri huwo umwtolewa na Ustadh Ali Nassor Abdallah wakati akifungua Madrasa ya Quran huko katika kijiji cha Uwaani Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema Quran ndio msingi mkuu wa maisha hivyo kukisoma ni wajibu mkubwa kwa waislam na ndio ngao ya kuingilia peponi.

Amefahamisha kuwa kujengwa kwa madrasa katika maeneo hayo kutaweza kuwaondolea usumbufu watoto wao na hata watuwazima  kupata sehemu mzuri ya kukisoma kitabu cha Allah na kuondokana na usumbufu wa kwenda masafa marefu hali iloyochangia kukosa muda kabisa wa kujisomea.

Ameeleza kuwa inapaswa kuwashukuru wale wote waliochangia  ujenzi wa madrasa hiyo kwani wameonesha moyo ya kujitolea hivyo nivyema kwa wakaazi wa eneo hilo kuithamini na kuienzi ili iweze kuleta matunda mazuri kwa maslahi ya dunia na akhera pia.

Aidha amewataka wafadhili walio jenga madrasa hiyo kuweza kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kuwatafutia walimu ambao wataleta msukumo mkubwa katika ufundishaji .
Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji  hao Ali Khamis Mbarouk amesema  ujenzi wa madrasa hiyo utawesaidia kwa asi limia kubwa watoto wao kupata elimu kwa ufanisi na kwawakati muafaka.

Ujenzi wa madarsa hiyo umefadhiliwa na taasisi ya Istiqama Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Comments