Wafungwa hao wametangaza kwamba, hatua ya kufungwa katika jela hiyo ya mateso ni kinyume cha sheria na imetokana tu na wao kuwa Waislamu si vinginevyo.
Kadhalika wamesisitiza kwamba hatua za uhasama za kiongozi huyo wa marekani ikiwa ni pamoja na kutoa amri dhidi ya wahajiri inayowapiga marufuku Waislamu wa nchi sita kuingia Marekani na kadhalika maandishi ya mara kadhaa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter dhidi ya Waislamu, vinabainisha ni kwa kiasi gani Trump alivyo na chuki ya hali ya juu dhidi ya Uislamu.
Awali rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliahidi kuifunga jela ya Guantanamo.
Hata hivyo Trump alipinga suala hilo na kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwake.
Trump pia ametaka kuongezwa mateso kwa wafungwa wa jela hiyo na jela nyingine zilizo chini ya udhibiti wa Marekani duniani.
Hivi karibuni Mwasisi wa Baraza la Mahusiano la Kiislamu nchini Marekani (Council On American-Islamic Relations) alilisisitiza kwamba, tangu Trump alipoingia White House, vitendo vya chuki na ubaguzi dhidi ya Uislamu na Waislamu vimeongezeza zaidi.
Ibrahim Hooper sambamba na kuashiria kwamba kuingia madarakani Trump nchini Marekani kumekuwa sababu ya wazungu wabaguzi kushadidisha wimbi la mashambulizi yao, amesema kuwa matamshi ya rais huyo yameiingiza Marekani katika hatua mpya.
Hooper ameongeza kwamba, vitendo vya ubaguzi na chuki haviwalengi Waislamu pekee, bali watu wa matabaka yote nchini Marekani hivi sasa wanapitia wakati mgumu ndani ya nchi hiyo inayojinadi kuwa eti ni mtetezi wa haki za binaadamu duniani.
chanzo:parstoday.
Comments