UN yalaani hatua ya Israel ya kuwafukuza wahajiri wa Kiafrika.

UN yalaani hatua ya Israel ya kuwafukuza wahajiri wa KiafrikaUmoja wa Mataifa umeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kufuta mpango ulioanza kuutekeleza hivi karibuni wa kuwarejesha nchini kwao kwa nguvu makumi ya maelfu ya Waafrika walioingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu.

William Spindler, msemaji wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja UNHCR jana Jumanne aliwaambiwa waandishi wa habari mjini Geneva kuwa, mpango huo sio wa kueleweka na umekuwa ukitekelezwa kwa njia isiyokuwa ya uwazi.
Amesema kutoka na ukweli kwamba nchi zinazodaiwa kuridhia kuwapokea wahajiri hao zimekanusha jambo hilo, ni jambo linaloutia wasiwasi umoja huo na inakuwa vigumu kwao kuweza kufuatilia.
Hivi karibuni serikali za Uganda na Rwanda zilikanusha hadharani taarifa za kukubali kuwapokea maelfu ya wahajiri wa Kiafrika kama sehemu ya mpango uliofikiwa baina ya nchi hizo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Jumatano iliyopita, utawala wa Kizayuni wa Israel ulianza kutekeleza mpango wa kuwarejesha nchini kwao kwa nguvu makumi ya maelfu ya Waafrika walioingia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu.
Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema wahajiri haramu 38,000 wa Kiafrika wana muda wa hadi mwezi Machi mwaka huu kuondoka kwa khiari, vinginevyo watakamatwa.
chanzo:parstoday.

Comments