Imeelezwa kuwa vitendo vya
udhalilishaji vimekuwa vikiendelea katika jamii Licha ya serikali kupambana na
suala hilo.
Wakizungumza baadhi ya wakaazi wa
dunga wamesema vitendo vya udhalilishaji vimeenea katika jamii jambo ambalo
inawarejesha nyuma kimaendeleo.
Nae Salma Sleiman kutoka jumuiya ya wanasheria wanawake zanzbar
amesema wameamua kuandaa mpango wa utoaji elimu kwa ili
kuwa na uwelewa kuhusu vitendo vya udhalilishaji.
Pamoja na hayo ameiomba jamii
kuachana na muhali na badala yake watoe ushirikiano ili kutokomeza vitendo vya
udhalilishaji nchini.
Comments