Lam Paul Gabriel msemaji wa Jeshi la Ukombozi wa Sudan Kusini ameeleza kuwa washirika wa kimataifa wa amani ya nchi hiyo na baadhi ya viongozi wa ndani huko Sudan Kusini wameendelea kukiuka vipengee vya makubaliano mapya ya amani.
Gabriel ameituhumu Troika hiyo katika mchakato wa amani wa Sudan Kusini kwa kushadidisha machafuko na mapigano nchini humo.
Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi ya nchini humo mwezi Disemba mwaka jana yalisaini makubaliano mapya ya amani huko Addis Ababa Ethiopia kwa lengo la kuhitimisha mapigano nchini humo.
Sudan Kusini hivi sasa imetumbukia katika vita vya ndani baada ya miongo kadhaa ya mivutano na kujitenga na Sudan mwaka 2011.
chanzo:parstoday.
Comments