
Mkufunzi
wa Arsenal Arsene Wenger anatarajiwa kuilipa Boca Juniors kitita cha
pauni milioni 27 kumsajili Cristian Pavon katika ligi ya premia. (TyC
Sports - in Spanish)
Wakati huohuo, Wenger anatarajiwa kukaa
katika viti vya mashabiki katika uwanja wa Stamford Bridge kwa mechi ya
Jumatano ya nusu fainali ya kombe la Carabao baada ya kupigwa marufuku
ya kukaa katika eneo la wakufunzi (Express)
Mkufunzi wa Real
Madrid Zinedine Zidane anasema kuwa hataki kuwasajili wachezaji wapya
katika dirisha la uhamisho licha ya kuwa nyuma ya viongozi wa ligi ya La
Liga Barcelona.. (Reuters)
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaondoka Old Trafford kabla ya kukamilika kwa msimu huu.
Raia huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 36 hana kandarasi na klabu hiyo. (Yahoo Sport)
Everton
imetoa chanagamoto kwa Southampton katika ushindani wa kumsajili
mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 28, kwa dau la £20m. (Mail)
Liverpool na Arsenal watalazimika kulipa takriban £90m kumsajili mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 22. (Mirror)
Lakini
kulingana na mwandishi wa Ufaransa Julien Laurens, huenda akachelewesha
uhamisho wake Liverpool kutokana na michuano ya kombe la dunia (5
live's Euro Leagues podcast)
Winga wa Brazil Lucas Moura, 25,
amekubali kujiunga na Manchester United kutoka Paris St-Germain,
ijapakuwa kitita cha uhamisho huo hakijakubalika kati ya vilabu hivyo
viwili. (Gazetta dello Sport - in Italian).
Arsenal itawasilisha rasmi ombi jipya la kandarasi mpya ya kiungo wa kati wa Uingereza Jack Wilshere.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuanza mazungumzo na Arsenal
katika kipindi cha wiki moja ijayo na atalazimika kupunguza mshahara
wake ili kusalia klabu hiyo. (Mirror)
Borussia Monchengladbach bado imejiandaa kumsajili beki wa West Ham Reece Oxford.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 19 aliichezea mara nne klabu hiyo wakati
alipokuwa katika mkopo lakini alirudi katika klabu yake mwezi Disemba.
(Borussia Monchengladbach).
Na West Ham huenda ikamuuza beki wa Uingereza iwapo ligi ya Bundesliga imejiandaa kuongeza ombi lake la £15m. (Telegraph).
Klabu ya Uhispania ya Sevilla ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 24, kwa mkopo. (ESPN).
Lakini
mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amesema anafuraha anampenda mchezaji
huyo wa Ubelgiji ambaye ameichezea Chelsea mara mbili pekee. (Sky
Sports).
chanzo:Bbc.
Comments