
Maamuzi hayo yamekuja baada ya Waziri Kigwangalla mwezi uliopita
kufanya ziara ya kushitukiza bandarini hapo baada ya kupata taarifa kuwa
kuna shehena hiyo ya magogo ambayo umiliki wake ulikuwa na utata.
Mhe. Kigwangalla alieleza kuwa magogo hayo yamekuwa bandarini kwa miaka 10 huku mengine yakiwa kwenye makontena 55 .
Kutokana na utata huo, Kigwangalla alitoa siku 30 kwa wamiliki wa
makontena 55 kujitokeza wakiwa na nyaraka zote ili kuthibitisha kama
kweli yalivunwa Zambia kama ilivyodaiwa au laah!.
“Kulikuwa na vikao mbalimbali ndani ya serikali kujadili
suala hilo, na tumekubaliana kuyauza baada ya wahusika kutojitokeza
kuthibitisha umiliki wake,” amesema Waziri Kigwangalla.
Waziri Kingwangalla amesema jukumu la kuyauza magogo hayo wamepewa
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaoruhusiwa kisheria kufanya kazi hiyo,
ambapo watashirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS).
chanzo: zanzibar24.
Comments