Akizungumza jana Jumatano hapa Tehran na Nabih Berri Spika wa Bunge la Lebanon, Rais Hassan Rouhani alibainisha kuwa katika miezi ya hivi karibuni sura halisi za baadhi ya serikali za eneo la Mashariki ya Kati zimefahamika vyema na akasema anataraji kuwa nchi zote za eneo hili zitastafidi na uwezo wao kuimarisha uthabiti, usalama nan umoja kati yazo na kutotoa mwanya kwa madola ajinabi khususan utawala wa Kizayuni na Marekani kufanikisha njama zao za kuzusha migawanyiko katika eneo.
Rais Rouhani amebainisha kuwa hii leo nchi za Kiislamu zina wajibu wa kushughulikia masuala mbalimbali ya Ulimwengu wa Kiislamu kuliko ilivyokuwa huko nyuma na zinapasa kuzidisha ushirikiano wao.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa mustakbali mwema unaweza kuandaliwa kwa ajili ya eneo hili iwapo kutakuwepo umoja, jihad na jitihada.
Katika mazungumzo hayo Spika wa bunge la Lebanon Nabih Berri amefafanua hali ya mambo ya nchi hiyo na kuipongeza Iran kutokana na uungaji mkono wake kwa mapambano na muqawama wa wananchi na Harakati ya Hizbullah ya nchi hiyo mbele ya utawala wa Kizayuni.
Nabih Berri amebainisha kuwa leo hii kuna umoja na mshikamano mzuri huko Lebanon na kuongeza kuwa Iran imekuwa na nafasi chanya katika kuipatia ufumbuzi migogoro mbalimbali katika nchi za eneo hili.
Spika wa Bunge la Lebanon amefanya safari hapa Tehran kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 13 wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa OIC.
chanzo:parstoday.
Comments