Rais Rouhani: Umoja wa Wairani dhidi ya wafanya fujo, ushindi mwingine mbele ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu.

Rais Rouhani: Umoja wa Wairani dhidi ya wafanya fujo, ushindi mwingine mbele ya maadui wa Jamhuri ya KiislamuRais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kujitokeza kwa wingi sana wananchi welewa, umoja ulioonesha na mirengo yote nchini pamoja na watu wa kaumu na madhehebu yote kukabiliana na wafanya fujo, ni ushindi mwingine kwa Iran katika kukabiliana na maadui wa Jamhuri ya Kiislamu.

Rais Rouhani amesema hayo usiku wa kuamkia leo katika kikao cha Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiutamaduni na sambamba na kuwahimiza viongozi wenzake kuongeza juhudi za kutatua matatizo ya wananchi na kutekeleza matakwa yao ya haki amesisitiza kuwa, welewa uliooneshwa na wananchi wa matabaka mbalimbali na watu wa vyuo vikuu, umeonesha kuwa wananchi wa Iran hawako tayari kutumiwa vibaya na maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Vile vile amevishukuru vikosi vya ulinzi kwa hekima viliyotumia katika kuamiliana na matukio ya hivi karibuni humu nchini na kusema, vikosi hivyo vimetekeleza vizuri majukumu yao bega kwa bega na wananchi.
Rais Rouhani amezungumzia pia kutimia mwaka mmoja tangu alipofariki dunia Ayatullah Hashemi Rafsanjani, Spika, Rais Mstaafu na Mkuu wa zamani wa Halmshauri ya Kuainisha Maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema kuwa, Ayatullah Rafsanjani alikuwa shakhsia mkubwa ambaye aliheshimiwa na wananchi na hata jamii ya kimataifa. 
chanzo:parstoday.

Comments