
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Uhamiaji ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa
Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda katika mahojiano maalum na Idara ya Habari
(MAELEZO).
Mtanda amesema kuwa Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki ni
sehemu ya Mfumo wa Uhamiaji Mtandao ambao utakuwa na visa, vibali mbali
mbali na manejimenti mipakani.
Kwa kuwa teknolojia inazidi kukua, Tanzania haiwezi kubaki nyuma ndiyo maana imeamua kuingia katika masuala ya digiti.
Uzinduzi huu utahudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waheshimiwa, Ali
Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete na
viongozi wengine wa Serikali wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo kwa
mujibu wa Mtanda.
Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati katika kutoa huduma zake kwa wananchi kwa njia ya mtandao.
Ikumbukwe kuwa usajili wa makampuni chini ya Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA) wamezindua usajili wa makampuni kwa njia ya
mtandao, miamala ya pesa inafanyika kwa kiwango kikubwa kwa njia ya
mtandao na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi ikiwepo kulipa kodi
mbali mbali.
chanzo: zanzibar24.
Comments