Vijana watakiwa kuwa kitu kimoja kuleta maendeleo.

File:Chama Cha Mapinduzi Logo.png

Na Hamida Mohd Abdalla.

Vijana wa Jimbo la Amani Shehia ya kwa Wazee wametakiwa kuwa kitu kimoja katika kuendeleza maendeleo yanayopatikanwa ndani ya shehia  kutoka kwa viongoz wao.

Yameelezwa hayo na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya kwa wazee salmin Mussa Nahoda huko ofisini amesema kuwa vijana wawe kitu kimoja bila kubaguana na itikadi za chama, rangi, kabila na hata dini.

Aidha  amewataka wazazi na walezi kuwa sio vyema kuyatumia mabaraza ya vijana kwa itikadi ya kisiasa,  kwani maendeleo wanayoyapata ni kwa ajili ya wanachi wote wa jimbo na sio chama fulani.

Kwa upande wake Katibu wa baraza hilo Harouna Ali amesema  ni vizuri kuzitumia fursa zinazotokea ndani ya shehia yao na kuendeleza miradi inayotolewa ili kujikwamua na umasikini .

Hidaya Hassani ni mmoja wapo aliejiunga ndani ya baraza hilo na kusema kuwa hawatoacha kuwaunga mkono viongozi  wao kwani wamepata fursa nyingi kwa vijana wa shehia hio.

Ametoa wito kwa vijana ambao hawajiunga na mabaraza ya vijana, kuwa mabaraza yana faida nyingi kwao ni vyema n wao wakaajiunga ndani ya majimbo yao.

Comments