Sadr ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter
kuwa, "Kwa mara nyingine tena vikosi vamizi vya Marekani vimedhihirisha
ukatili na kiburi chao kwa kukanyaga uhuru wa kujitawala wa serikali na
taifa la Iraq."
Kiongozi huyo wa Kiislamu nchini Iraq amesema shambulizi la anga la
hivi karibu lililopelekea kuuawa askari 10 na raia mmoja wa Iraq mkoani
Anbar ni muendelezo wa tabia ya Washington ya kukiuka uhuru wa
kujitawala Iraq.
Wakati huo huo, Qais al-Khazali, kamanda wa ngazi za juu wa vikosi
vya kujitolewa vya wananchi vya Hashdu-Sha'abi amesema hujuma hiyo ya
anga ya jana ya Marekani imeibua masuali mazito kuhusu lengo la uwepo wa
jeshi la Marekani nchini Iraq.
Licha ya jeshi la Iraq kutangaza habari ya kutamatisha operesheni
dhidi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) mwezi uliopita,
lakini muungano wa kijeshi wa Marekani unaendelea kutafuta vijisababu
vya kusalia katika nchi hiyo ya Kiarabu yenye utajiri wa mafuta.
chanzo: parstoday.
Comments