Mgombea
wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Maulid Said Mtulia amesema amefanya
maamuzi ya kiume ya yeye kuhamia chama hicho kwa sasa kwa maana wapo
wengi wanataka kufanya hivyo lakini wameshindwa kwa madai wanasubiri
kulipwa kiiunua mgongo.
Mtulia
ameeleza hayo wakati alipokuwa anaendelea kujinadi kwa wananchi wa
jimbo la Kinondoni ambalo hapo awali alikuwa analishikilia yeye kupitia
chama chake cha CUF kabla ya kujivua uanachama wake na kuenda kumuunga
mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kuijenga nchi.
"Kujiuzulu
Ubunge sio mchezo, nimefanya maamuzi ya kiume maana kuna wenzangu
wengine mpaka sasa hawawezi kutoka kwa sababu wanasubiri kiiunua mgongo.
Sasa kijana kama mimi nikae pale nisubirie kiunua mgongo hivi kweli
ntaweza kuishi kwa kusubiri kiiunua mgongo", alisema Mtulia.
Aidha,
Mtulia amesema amejinusuru kwa mengi kukihama chama chake cha awali ili
aweze kuwapigania wananchi wa jimbo hilo kwa maana hapo awali alikuwa
anashindwa kuyafanya majukumu yake vizuri kutokana na mgawanyiko ndani
ya chama chao.
"Wenzangu
Wabunge 10 walifukuzwa uanachama CUF hamkujua, mlisubiri nifukuzwe au
mna roho mbaya na mimi. Hivi nilipo hapa nimeruka kwa kujinusuru
nashukuru nipo salama na nimesimama tena kwa wana kinondoni ninaomba
kugombea Ubunge nyie mnanuna kitu gani au huo ndio usaliti. Lakini jambo
jingine mimi nimekuja CCM kwa sababu nampenda Magufuli balaah", aliuliza Mtulia.
Pamoja
na hayo, Mtulia aliwashangaza baadhi ya watu kwa kusema ametumikia
Ubunge ndani ya miaka miwili na kushiriki vikao vyote vya Bunge lakini
hakuweza kuwa na namba ya Rais Magufuli.
"Leo
ninawaambia siri yangu, nilivyokuwa Mbunge miaka miwili namba ya Rais
Magufuli sikuwa nayo lakini sasa namba ninayo. Hivyo wanakinondoni
mnataka nini kama mnataka maendeleo ndio haya", alisisitiza Mtulia.
Kwa
upande mwingine, Mtulia amewaambia wananchi wa Jimbo la Kinondoni
endapo watamchagua yeye katika chaguzi hizo za marudio zilizopangwa
kufanyika mapema Februari 17 mwaka 2018 basi watakuwa wametengeneza
daraja la kujipatia maendeleo.
chanzo:Mpekuzi.
Comments