Mbunge huyo maarufu kwa jina la Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 30,2017 katika mkutano wa hadhara walioufanya kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.
Kesi hiyo inaendelea leo Alhamisi Januari 25,2018 kwa washtakiwa kutoa ushahidi.
Washtakiwa wanawakilishwa na mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite.
chanzo:Mwananchi.
Comments