
Mfungwa Gonzalo Montoya Jiménez alikuwa kuzuizini katika gereza moja
jimbo la Asturias na alizinduka saa chache kabla ya kufanyiwa upasuaji
ili kubainisha chanzo cha kifo chake ambapo mwili wake tayari ulikuwa
umechorwa alama tayari kwa upasuaji.
Kwa sasa, amewekwa chini ya uangalizi wa madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Oviedo.
Mmoja wa jamaa zake ameambia gazeti la La Voz de Asturias kwamba Montoya “alikuwa na alama ya kufanyiwa upasuaji, tayari kupasuliwa”.
Inadhaniwa kwamba hicho kilikuwa kisa cha hali iitwayo ‘catalepsy‘ duru katika hospitali hiyo zimeambia runinga ya Telecinco ya Uhispania.
Catalepsy ni hali ambapo ishara muhimu za uhai kwenye mwili wa binadamu hufifia kiasi cha kutoweza kutambulika.
Hata hivyo, hili bado halijathibitishwa.
“Kifo” chake kilikuwa kimethibitishwa na madaktari watatu gerezani
ambao waliagiza mwili wake upelekwe kwenye ufuo kwa uchunguzi zaidi.
Mwili huo ulipelekwa ufuo wa Taasisi ya Matibabu ya Kisheria katika makao makuu ya jimbo Oviedo.
chanzo: zanzibar24.
Comments