Wazazi na walezi wametakiwa kuongeza
ushirikiano kwa walimu ili kupeleka mbele
maendeleo ya elimu kwa watoto wao.
Akizunguma na NOCOMPED MEDIA msimamizi wa skuli ya the world talent iliyopo jangombe Juma Muhammed Mzee katika mahafali ya skuli hiyo amesema
wanakabiliwa na changamoto ikiwemo baadhi ya wazazi kutolipa ada skulini hapo
jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya skuli hiyo.
Kwaupande wao baadhi ya wanafunzi waliopewa vyeti kwa somo la
kiengereza wamesema wamefaidika vya
kutosha kupitia mafunzo ya lugha hiyo.
Hata hivyo wamewashauri wanafunzi wenzao kutokata tamaa katika
kutafuta elimu na badala yake wafanye
bidii ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Comments